"MAISHA NI NYUMBA NA NYUMBA NI MSINGI"
Luka 6:46-49
Sehemu
ya I
Bwana Yesu asifiwe!
Ndungu
msomaji wangu nakusalimu katika Jina la Yesu. Ni muda mrefu lidogo tangu
niandike ujumbe wa kukutia moyo katika blogu hii ya ONLY BELIEVE! (AMINI TU!). Hata hivyo namshukuru Mungu kuwa
nimerejea tena.
Upo
msemo mmoja ambao umekuwa ukitumiwa sana na shirika moja la umma nchini
Tanzania katika kunadi bidhaa zake. Msemo huo husemwa hivi: "Maisha ni Nyumba"- wakimaanisha
kuwa kama hujajenga nyumba basi maisha yako yako katika hati-hati ya mahangaiko
ili-hali wao wanaweza kukupatia nyumba ya bei nafuu kabisa, ukaishi maisha
yenye utulivu, ukapanga mipngo yako na kuendelea mbele kimaisha. Kwa hali hiyo
wao hujinadi kwa kusema : Maisha ni
nyumba!
Katika
hali ya kuutafakari msemo huo ndipo nilipopata nafasi ya kulitafakari Neno la
Mungu lisemavyo na kuona kuwa maisha ya mtu wa Mungu, mtu wa roohoni yaani Mkristo
ni Nyumba inayojengwa kila siku na Numba inakuwa Nyumba kutokana na Msingi
wake. Hivyo Nyumba ni Msingi. Kulianagali
jambo hilo kimaandiko na kuona ni jinsi gani tunapaswa kuyajenga maisha yetu ya
Ki-kristo, tuangalie Maandiko Matakatifu katika Injili ya Luka 6:46-49.
Yesu
alifundisha akisema maneno haya:
"Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?
Kila mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda,
nitawaonyesha mfano wake. Mfano wake ni mtu ajengaye nyumba, na kuchimba
chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika, mto uliishukia nyumba ile
kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Lakini yule aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni
mtu aliyejenga
nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na
msingi, mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba
ile yakawa makubwa."
Kwa
kuchukulia ule msemo wa 'maisha ni
nyumba' na kwa kuyaangalia maandiko
hayo yaliyonukuliwa hapo juu, utaona kwamba nyuma ni MSINGI. Bila kuwepo kwa
msingi imara nyumba yoyote ile inayojengwa itaanguka tu- kama si leo basi baada
ya muda si mrefu! Hili latufundisha nini basi?
Maisha
yetu ya Ki-kristo yanafananishwa na nyumba inayojengwa. Mjenzi ni wewe au mim
mwenyewe. Kila siku tunaijenga nyumba hii lakini ujenzi huu uko wa aina mbili ,
yaani ipo tofauti katika kujenga kwetu.
Kwa
upande mmoja wapo wale ambao wanajenga maisha yao ya kila siku juu ya msingi
ulio imara, usioweza kutikiswa na kitu chochote- yaani wanajenga juu ya NENO LA MUNGU. Neno la Mungu yaani "Biblia"
ni mwamba ulio imara sana ambao hauwezi kutikisika au kutikiswa na jambo lalote
au halitabia yoyote. Hii ni kutokana na tabia ya Neno lenyewe.
Kataka Zaburi ya 12:6 Biblia inasema hivi kwa
habari ya uthabiti wa Neno la Mungu. Inasema, nami nanukuu:
"Maneno ya
BWANA ni maneno safi. Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; iliyosafishwa
mara saba."
Mithali 30:5 inasema
"Kila Neno la Mungu
limehakikishwa.
Zabiri 18:30 yasema:
"Ahadi ya BWANA
imehakikishwa".
Katika
kujenga maisha thabiti juu ya NENO la Mungu, Yesu alifundisha pia juu ya mambo
kadhaa muhimu kuyazingatia na kujipima kwayo kadri tunavyoenenda siku kwa siku.
Moja ya mambo haya ni 'Kusikia Neno'
na 'Kulitenda Neno'.
Kusikia Neno : hii ni hatua ya
awali sana katika kujemga maisha ya Kikristo yenye matunda, kwa mtu anayemjia
Kristo, yaani mtu aliyeokoka. Ni vizuri, tena ni muhimu kulisikia Neno
linavyosema na maisha yako au yangu , tena tulisikie kwa 'sikio la ndani' sana, yaani sikio
la rohoni. Biblia inasema tulisikiapo Neno huleta kuliamini au Imani.
Warumi 10:17 inasema:
"Basi imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja
kwa Neno la Kristo".
Hivyo,
kulisikia Neno la Kristo huleta
kujengewa imani ndani yetu. Lakini kusikia tu haitoshi maana imani yapaswa kuwa
na mizizi ndani ya mtu kwani tunakua na kuongezeka toka imani hata imani!
Katika hili la kusikia kuna hatua ya ziada ambayo inaambatana na sio
tu kusikia bali pia kulielewa Neno. Mtu aliyelisikia tu
Neno la Mungu lakini asichukue hatua zaidi ya kutaka kulielewa Neno alilolisikia
na kulipokea hatafaidika au halitamfaida kitu.
Yesu
aliliweka bayana jambo hili katika Injili ya Luka 8:4-15 aliopoutoa mfano wa
Mpanzi aliyekwenda kupanda mbegu. Mistari ile ya 11 hadi 15 Yesu anatoa
ufafanuzi wa mfano alioutoa kwa wanafunzi wake. Katika tafsiri ile Yesu
anaonesha waziwazi kuwa mtu anaweza kulisikia Neno la Mungu nalo likamfaidia au
lisimfaidie kabisa.
Luka
8:11-12 Yesu anasema hivi:
"Mbegu ni Neno la Mungu. Wale waliopandwa
karibu na njia ndio wasikiao kisha huja Ibilisi akaliondoa hilo Neno mioyoni mwao
wasije wakaamini na kuokoka."
Kama
utakavyoona hapo juu, lengo la Neno la Mungu ni kumwokoa yule anayelisikia.
Humpa mtu msaada wa kuvuka toka ng'ambo moja hadi ng'ambo ya pili. Yaani kutoka
mautini kuingia uzimani (Yohana 5:24).
Lakini ili hilo litimie kuna kuliamini Neno, jamba ambalo hija kwa kulisikia
lakini si tu kulisikia bali na kutafuta kulielewa ili kuendelea kukaa katika
hilo lililosikiwa bila kulionea mashaka. Kama mtuakisikia tu halafu asiendelee
nalo, Yesu alitahadharisha kuwa "huja yule mwovu akaliiba, akaliondoa moyoni
mwa mtu huyo" ili asije akaliamini na kuokolewa.
Kwa hiyo basi: 'Kusikia tu neno hakutoshi, tafuta kulielewa
Neno la Mungu!'
Tutaendelea
tena tukijaaliwa neema!
Barikiwa sana na
Bwana.
Ni mimi nduguyo katika
Kristo, Mchungaji Dkt.Deo John Nangela